Stori: Issa Mnally na Dustan Shekidele, Morogoro
OPARESHENI Fichua Maovu (OFM) ya Global
Publishers si mchezo! Safari hii imenasa tukio la
mchumba wa mtu aliyetajwa kwa jina moja la
Jose kuuza mwili.
Tukio hilo lilijiri eneo maarufu la Baa ya Kaumba
iliyopo katikati ya mji kwenye Mtaa wa
Makongoro, mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo
OFM na polisi walikuwa kwenye oparesheni za
kufichua uovu wa biashara haramu ya ngono.
Kwa mujibu wa mchumba huyo katika mahojiano
na OFM, aliaga kwao Kilosa kuwa anakwenda
Morogoro mjini kumuuguza bibi yake ambaye ni
mgonjwa. Tofauti na matarajio ya familia yake, mrembo huyo
alikwenda kukita kambi maeneo hayo akijihusisha
na biashara hiyo haramu eti kwa madai ya
kusaka fedha ya kununulia sare za harusi yake
ambayo inatarajiwa kufanyika Februari 15, mwaka
huu.
Jumatano iliyopita, OFM ilipokea simu kutoka kwa
dada mmoja ambaye alieleza kuwa kuna ‘shori’
ambaye ni mchumba wa mtu anajiuza katika
viunga vya Kaumba.
Dada huyo aliendelea kueleza kuwa yeye ni
mmoja wa wajumbe katika kikao cha harusi ya
dada huyo huku akiwa ameshachangia shilingi
elfu 50 lakini alishangaa kumuona maeneo hayo
hatarishi.
“Niamini mimi, tunakaa naye Mji Mpya
(Morogoro). Hata fedha za advance ya ukumbi,
vinywaji, MC na muziki tumeshalipa na harusi
yake inatarajiwa kufanyika Februari 15, mwaka
huu.
Baada ya kunyetishiwa habari hizo, kikosi kazi
cha OFM kiliingia mzigoni kwa kushirikiana na
dada huyo ambaye alivalishwa ‘beji’ yao na
kufanikisha kunaswa kwa mchumba huyo.
OFM ikishirikiana na polisi wanaojua kujituma
kwenye majukumu yao walimtia mbaroni dada
huyo akiwa katika pilikapilika zake za kunasa
wanaume huku mmoja wa vijana wa OFM
akijifanya mteja na kupatana naye bei ya kuingia
chumbani kwa ‘shoti taimu’.
Baada ya kunaswa, mwanadada huyo alikiri mbele
ya OFM kuwa ni bibi harusi mtarajiwa.
“Jamani… jamani ni kweli mimi ni mchumba wa
mtu, shetani ameniponza nisameheni,” alisema.
Hata hivyo, kilio chake kiligeuka cha samaki
kwani hakikusikika, yeye na wenzake walionaswa
walipelekwa moja kwa moja katika kituo kikuu cha
polisi ili kupisha sheria ichukue mkondo wake.
---gpl--