Kabang! Memba wa Kundi la Tip Top Connection lenye maskani yake Manzese jijini Dar, Khalid Ramadhan ‘Tunda Man’ na mwanamuziki wa nchini Kenya, Mwanaisha Abdallah ‘Nyota Ndogo’ wamenaswa laivu wakiwa kwenye pozi la mahaba niue.
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini kutoka nchini humo, wawili hao walikuwa wakijiachia nyumbani kwa Nyota Ndogo huku kukiwa na madai mazito kuwa eti wanapika na kupakuwa.
Ilidaiwa kwamba Tunda Man anapokwenda Kenya huwa anafikia nyumbani kwa Nyota Ndogo. “Wasanii wengi wanakuja Kenya wanajifanya kuja kufanya shoo kumbe wanawafuata wanawake zao ila mimi namsihi Tunda Man ajiangalie, yasije yakamkuta kama ya wasanii wengine walivyopewa masaa ishirini na nne wasikanyage Kenya tena,” kilisema chanzo hicho.
“Kaka nadhani unajua kuwa nina mke na sijawahi kupata skendo kubwa kama hiyo, Nyota Ndogo namheshimu kama dada yangu na sijawahi hata kufikiria kumtongoza please achana na hiyo habari,” alijitetea Tunda Man bila kujua tuna picha zao za mahaba.