Msanii Johari Blandina ‘Chagula’ ambaye
ni star mkongwe Swahiliwood amesema
kuwa anamshukuru Mungu kwa kuutunza
muonekanio wake na kuwa kama kijana
licha ya umri wake kuwa mkubwa tofauti
na baadhi ya waigizaji wenzake wa kike
ambao hujiachia na kuonekana wazee
licha ya umri wao kuwa mdogo.
Akizungumza na Filamucentral Johari
alisema:
“Wasanii wa kike wengi ni watoto wadogo
lakini kwa sababu ya kujiachia
wanaonekana kama watu wazima lakini
ukweli ni watoto wadogo sana, namshukru
Mungu nimeanza sanaa kitambo lakini
mwili wangu upo fiti,”
Johari alimtolea mfano Irene Uwoya
ambaye ni shoga’ke wa karibu kuwa
anaonekana mkubwa kwasasa sababu ya
kujiachia licha ya kwamba amempita
miaka kadhaa. Vile vile Johari amesema kuwa kawasasa
amerudi kwa moto wa kasi kama
muigizaji kama awali baada ya kuwa
upande wa producer kuwapa nafasi
chipukizi ambao wengi amesema
wameshindwa, hivyo amerudi mwenyewe
kwenye game.