Featured Posts

Friday, August 1, 2014

SOMA HAPA UKWELI KUHUSU YULE MWANAUME LIYEZAMISHWA SHOKA KICHWANI

KATIKA Gazeti la Risasi Jumamosi Toleo la Julai 26, 2014 ukurasa wake wa mbele kulikuwa na kichwa cha habari kisemacho;
Bw. Oka Constantine (35) akiwa amejeruhiwa na sururu.
TUKIO LA KUTISHA!
Habari hiyo ilimhusu mwanaume mmoja ambaye jina halikupatikana kuwa alipigwa shoka (baadaye ilibainika ni sururu) hadi kuzama kichwani upande wa kushoto kwa madai ya kufumaniwa na mke wa mtu katika eneo ambalo pia halikujulikana.
Kingine katika habari hiyo, haikujulikana mara moja mtu huyo alikumbwa na tukio hilo sehemu gani ya Tanzania lakini ilijidhihirisha kuwa ni hapa nchini kutokana na shuka alilofunikwa akiwa hospitali kuandikwa; MSD. MSD (Medical Stores Department) ni mashuka yanayotolewa na Serikali ya Tanzania kwenye hospitali zake.Picha ya X-ray ikionyesha surulu ilivyomjeruhi.
KILICHOBAINIKA
Siku chache baada ya habari hiyo kutoka gazetini imebainika kwamba, mwanaume huyo anaitwa Oka Constantine mwenye umri wa miaka 35, Risasi Jumamosi lina ‘full story’.
KUMBE NI BUGANDO
Habari za uhakika zinasema kuwa, Oka amelazwa katika Hospitali Teule ya Bugando Mwanza.
Akizungumza na gazeti hili juzi, mkurugenzi wa utawala na utumishi wa hospitali hiyo, Leah Kagine alisema hali ya Oka bado haijatengemaa kwani bado hana ufahamu wa kutambua wala uwezo wa kuzungumza.
“Huyo mtu aliyepigwa shoka yupo hapa Bugando, hali yake bado. Hana ufahamu, hawezi kuzungumza, labda urudi baada ya wiki mbili hivi unaweza kumkuta amepata fahamu,” alisema Kagine.
Madaktari wakifanya upasuaji kuokoa maisha ya Bw. Oka Constantine.
UKUBWA WA JERAHA
Kagine aliongeza kusema kuwa, kwa sasa bado ni vigumu kubaini ukubwa wa jeraha hadi daktari atakapotathimini na kuthibitisha kulingana na maadili ya kitabibu.
“Kuhusu ukubwa wa jeraha ni vigumu kwa sasa kuzungumzia hilo, hadi hapo daktari wake atakapofanya tathimini ya hali yake. Kisheria daktari ndiye anayeweza kuzungumza mara baada ya tathimini kufanyika,” alisema Kagine.
WALICHOKIFANYA MADAKTARI
Kwa mujibu wa mmoja wa madaktari wa kitengo cha dharura hospitalini hapo, Oka alifanyiwa upasuaji eneo la ubongo na kulazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi wanaohitaji uangalizi maalum (ICU).
Sururu iliyotolewa kutoka kwenye kichwa cha majeruhi.
MADAI YA KUPIGWA SHOKA
Kwa mujibu wa watu waliodai kumfahamu Oka, anatuhumiwa kupigwa shoka katika fumanizi na mke wa mtu na kupoteza fahamu hapohapo mpaka sasa.
ASILI YAKE
Uchunguzi wa kina uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa, majeruhi huyo ni mkazi wa Kijiji cha Miyombo, Kata ya Rwamgasa mkoani Geita.
KAZI YAKE
Ilizidi kudaiwa kuwa, Oka ni fundi wa mashimo ya dhahabu alikuwa akifanya kazi ya uchimbaji katika shimo Namba 41 ambalo kwa sasa limebadilishwa namba hiyo na kuitwa Namba 1.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, ACP Joseph Konyo.
SIKU YA TUKIO
Siku ya tukio, Oka alidaiwa kukutwa akiwa amekaa na mke wa mtu ndipo mwenye mke akachukua sururu maarufu kwa jina la moko na kumpiga nayo kichwani mpaka kuzama kisha akaondoka eneo la tukio kimyakimya, mkewe alishakimbia.
Baada ya kuanguka na kupoteza fahamu akiwa na damu chapachapa, wasamaria wema walimpeleka kwenye Kituo Kidogo cha Polisi cha Rwamgasa na kisha kukimbizwa Hospitali Teule ya Wilaya ya Sengerema (Sengerema DDH) ambako alipewa matibabu ya dharura na kumhamishia Bugando.
MAKAMANDA WANAVYOPITWA NA MENGI
Awali na kwa nyakati tofauti makamanda wa
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita: “Nimepigiwa simu na waandishi wengi wakiulizia tukio hilo. Niseme kwamba hapa mkoani kwangu halijaripotiwa. Kama lipo ningewaambia, siwezi kuficha jambo kama hilo.” Anaitwa  ACP Joseph Konyo.
Kaimu Kamanda Mkoa wa Mwanza, ACP Christopher Fuime: “Hakuna kitu kama hicho. Unajua watu wa mitandao ya kijamii wanachukua vitu na kuweka kwenye mitandao yao. Sijui hiyo wameitoa wapi?”

TUMEAMIA HUKU