Na Gabriel Ng’osha/GPL
MTANDAO wetu umevinjari mpaka wa Namanga ulioko Wilaya ya Longido, Mkoa wa Arusha, unaounganisha nchi ya Kenya na Tanzania na kugundua unazidi kuboreshwa kwa kujengwa majengo ya kisasa ambayo yatatumiwa na baadhi ya idara zinazofanya kazi katika eneo la mpaka huo.