STAA wa Bongo Fleva , Nasibu Abdul ' Diamond
Platnumz ' amemtupia vijembe mpenzi wake
Wema Sepetu kupitia ukurasa wake wa
Instagram usiku huu akionekana kuchukizwa
na tabia ya staa huyo kupenda maisha ya
starehe zisizo na faida . Katika ujumbe huo , Diamond ameandika kuwa
angewaona mashabiki wa mrembo huyo wana
akili na mapenzi ya dhati kama wangemshauri
apunguze mashoga wapenda anasa na kuacha
starehe zisizo na faida na kutumia fedha
kufanya mambo ya maendeleo kuliko
kuvifaidisha viwanda vya kutengeneza pombe .