Nicki Minaj anaendelea kuvuta umakini wa watu kuisubiria kwa hamu video ya wimbo wake ‘Anaconda’ ikiwa ni siku kadhaa baada ya kutoa kipande cha video kinachoonesha utengenezaji wake.
Jana August 18, 2014 Nicki ameshare picha nyingine za video hiyo inayomuonesha yeye akiwa amekaa katika mtindo wa mitego tata mbele ya Drake aliyekaa kwenye kiti.
Anaconda ni wimbo mpya unaotoka kwenye albam ya ‘The Pink Print’ na rapper huyo wa Young Money anatarajiwa kuuimba Live wakati wa utoaji wa MTV Video Music Awards, Jumapili, August 24.