Featured Posts

Sunday, September 14, 2014

YANGA YAICHAPA AZAM 3-0, YATWAA NGAO YA JAMII, TAZAMA PICHA ZOTE HAPA

Washindi wa Ngao ya Jamii 2014, Yanga SC.
Wachezaji wa Yanga wakiwa wamembeba juu kocha wao, Marcio Maximo baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Azam FC.
Wachezaji wa Yanga wakimpongeza Mbrazil, Geilson Santos 'Jaja' baada ya kufunga bao la pili.
Beki wa Yanga, Mbuyu Twite akiwa amembeba mfungaji wa bao la tatu la timu hiyo, Simon Msuva.
Wachezaji wa Azam FC wakikabidhiwa medali zao.
Haruna Niyonzima (katikati) akiwatoka wachezaji wa Azam FC.
Mrisho Ngassa (kushoto) akimtoka Michael Bollou wa Azam.
Jaja kazini.
Kikosi cha Azam kilichoanza mtanange huo.
Kikosi cha Yanga kilichoanza dhidi ya Azam FC.
KIKOSI cha Yanga SC kimetwaa Ngao ya Jamii baada ya kuichapa timu ya Azam FC mabao 3-0 katika mechi iliyopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam hivi punde.
Mabao ya Yanga yamefungwa na Geilson Santos 'Jaja' dakika ya 56 na 66 huku bao la tatu likiwekwa kimiani na Simon Msuva dakika ya 87 ya mchezo.
Hii ni mara ya pili Yanga kuifunga Azam katika mechi za Ngao ya Jamii baada ya msimu uliopita watoto wa Jangwani kuibuka na ushindi wa bao 1-0, mfungaji akiwa Salum Telela "Essien".

TUMEAMIA HUKU