Featured Posts

Sunday, September 14, 2014

YANGA YAICHAPA AZAM 3-0, YATWAA NGAO YA JAMII

KIKOSI cha Yanga SC kimetwaa Ngao ya Jamii baada ya kuichapa timu ya Azam FC mabao 3-0 katika mechi iliyopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam hivi punde.
Mabao ya Yanga yamefungwa na Geilson Santos 'Jaja' dakika ya 56 na 66 huku bao la tatu likiwekwa kimiani na Simon Msuva dakika ya 87 ya mchezo.
Hii ni mara ya pili Yanga kuifunga Azam katika mechi za Ngao ya Jamii baada ya msimu uliopita watoto wa Jangwani kuibuka na ushindi wa bao 1-0, mfungaji akiwa Salum Telela "Essien".

TUMEAMIA HUKU