Featured Posts

Thursday, September 18, 2014

USHAURI JAMANI: MAVAZI YA MKE WANGU YANANIPA WASI WASI NAISI MASHAROBARO WA TOWN WANAMLA URODA

MIMI naitwa 'John katuri' ni mkazi wa kiteto mkoani manyara, Ila kwa sasa nipo Arusha mjini nimehamishiwa huku kikazi.

Nimekuwa nikisumbuliwa sana na tatizo la mke wangu kuvaa viguo vya ajabu ajabu,
 

Kwakweli mimi sipendi kumbana kabisaa.. huwa napenda kumpa uhuru wa kuvaa mavazi ya aina hio kama mnavyoona hapo juu pichani. 


Muda wowote atakaojiskia kuvaa na wakati mwingine huvaa hivyo na kutoka mwenyewe kuelekea katika maeneo ya kujidai na kujirusha, Na ukizingatia mimi mara nyingi nashindwa kuongozana nae kwa kuofia miluzi na
 
makelele ya vijana mtaani kutokana na mavazi yake.
Kumwambia nashindwa maana nilimpata kibahatibahati kwa kuunganishiwa na mke wa rafiki yangu,


Kibaya zaidi nampenda kupita kiasi na yeye hunifokea pale napofanya jaribio la kumpangia aina ya mavazi ya kuvaa, Ila roho inaniuma..! Sijui ananisaliti? Naombeni ushauri jamani nifanyeje?

TUMEAMIA HUKU