Featured Posts

Wednesday, September 17, 2014

UKATILI ULIOFANYWA NA JWTZ KWA VIJANA WADAR ES SALAAM WAANIKWA HADHARANI, TAZAMA HAPA


KATIKA HALI ISIYO YA KAWAIDA, ASKARI WA JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA (JWTZ), WANADAIWA KUWAFANYIA UKATILI MKUBWA VIJANA 11, WAKAZI WA ENEO LA KEKO MAGULUMBASI B, WILAYA YA TEMEKE, DAR ES SALAAM KWA KUWAPIGA NA KUWALAZIMISHA WANYWE MAJI MACHAFU YENYE KINYESI.

Tukio hilo ambalo limefananishwa na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, linadaiwa kutokea Septemba 12 mwaka huu, saa 11 jioni, katika eneo la Keko Magulumbasi B.

Inadaiwa kuwa, wanajeshi hao ambao walikuwa saba wakiwa na sare za jeshi hilo, walifika Keko Magulumbasi B wakiwa na kijana mmoja mwenye asili ya Kiarabu na kuwavamia vijana waliokuwa wakila chakula kwenye kibanda cha chipsi.
Mashuhuda wa tukio hilo walidai kuwa, wanajeshi hao waliwakamata vijana hao na kudai wanahusika kupora simu ya kijana mwenye asili ya Kiarabu aina ya Tecno yenye thamani ya sh. 25,000.
Pamoja na vijana hao kukataa kuhusika na tukio hilo, waliwekwa chini ya ulinzi, kufungwa mikono kwa kamba, kulazwa kifudifudi na kuanza kupigwa mikanda ya jeshi.
Mashuhuda hao waliongeza kuwa, vijana hao walichukuliwa hadi kwenye bwawa la maji machafu yaliyochanganyika na kinyesi cha binadamu wakazamishwa vichwa vyao ndani ya bwawa hilo la kulazimishwa kunywa maji hayo.
Waliongeza kuwa, vijana hao wakiwa wameloana kwa maji machafu walichukuliwa na wanajeshi hao hadi Kituo Kidogo cha Polisi Keko na kuswekwa rumande na mmoja wao aliachiwa baada ya dakika 10.
Baadhi ya wakazi wa eneo hilo, walilazimika kuvamia kituo hicho na kufanya vurugu wakiwarushia mawe askari wa kituo hicho kwa lengo la kuwatoa vijana hao kwa nguvu wakidai wameonewa.
Hata hivyo, wananchi hao walitawanywa kwa risasi za moto zilizopigwa hewani na askari wa Kituo Kikuu cha Polisi Chang'ombe walioitwa kuongeza nguvu kituoni hapo.
Bw. Omary Abdu (30) ambaye ni mkazi wa eneo hilo ambaye alikuwepo kwenye eneo la tukio, alidai kutofurahishwa na kitendo kilichofanywa na wanajeshi hata kama vijana hao wameiba kwani walipaswa kufikishwa katika mamlaka husika ili hatua zichukuliwe.

CREDIT: AFRICANMISHE

TUMEAMIA HUKU