Featured Posts

Sunday, September 21, 2014

SHULE KIBAO ZA MSINGI DAR ZAFUNGWA, KUTOKANA NA KUIBIWA KWA WATOTO NA WATU WASIOJULIKANA

Uvumi wa kuwapo kwa watu wanaoteka nyara watoto kwa kutumia magari aina ya Noah, umeleta mtafaruku katika shule saba za msingi Manispaa ya Temeke, na kusababisha wazazi kuvamia shule hizo na kufungwa kwa muda.

Hata hivyo, katika baadhi ya shule hizo kumeripotiwa kutokea vurugu kiasi cha jeshi la polisi kuingilia kati kutawanya watu waliotaka kuvunja mageti ya kuingilia kwenye shule hizo.

Taarifa za kuwapo kwa matukio ya watoto kutekwa na watu wasiojulikana zilianza kuenea wiki tatu zilizopita, ambapo shule zilizoathirika ni Chekeni Mwasonga, Mikwambe, Rangi Tatu, Mchikichini, Charambe, Kiburugwa, Jitihada na Mbagala Kuu.

Akizungumza na NIPASHE Jumamosi, Afisa Elimu ya Msingi Manispaa ya Temeke, Honorina Mumba, alisema uvumi huo siyo wa kweli na hawafahamu nani anahusika kuusambaza na kwa madhumuni gani.

Alikiri kwamba kazi ya utoaji huduma katika baadhi ya shule umekuwa mgumu baada ya wanafunzi kutofika shuleni kufuatia  wazazi wao kuwazuia wakihofia usalama wa watoto wao.

TUMEAMIA HUKU