WAKATI serikali ikiwa katika utekelezaji wa mpango wa matokeo makubwa sasa, hali imeonekana kuwa tofauti katika shule ya sekondari Mwantini iliyopo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga mkoa wa Shinyanga baada ya kukutwa na waandishi wa habari wakifyatua matofali ya shule majira ya saa 5:00 asubuhi muda ambao wangetakiwa kuwa darasani wakiendelea na vipindi vya masomo. Wanafunzi hao wamekuwa wakifanya kazi hiyo wiki nzima bila kuingia darasani huku wakikosa masomo ambayo ni haki yao ya msingi.
Katika mahojiano na waandishi wa habari wanafunzi hao walisema wanasikitishwa na kitendo cha walimu kuwafanyisha kazi hiyo muda wa masomo wakati wengine wanajiandaa kuanza mitihani ya kidato cha pili na cha nne jambo ambalo linaweza kusababisha kiwango cha taaluma kushuka na kushindwa kufikia malengo ya matokeo makubwa sasa(BIG RESULTS NOW BRN).
Wanafunzi wakiendelea na kazi ya kuchanganya mchanga kwa ajili ya kazi ya kufyatua matofali.
|