Stori: Richard Bukos
Msanii nyota wa muziki wa kizazi kipya, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ juzikati alipata wakati mgumu baada ya mademu kumvaa na kutaka kumporomosha jukwaani wakati wa shoo ya Nani kama Mama iliyofanyika katika Ukumbi wa Mzalendo Pub, Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

Mashabiki wakimng'ang'ania msanii nyota wa muziki wa kizazi kipya, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ wakati wa shoo ya nani kama Mama.
Katika usiku huo, wiki iliyopita, Ommy Dimpoz alikuwa akimsindikiza Christian Bella, aliyekuwa akizindua albamu yake iitwayo Nani kama Mama.
Ommy Dimpoz alifanya makamuzi ya nguvu ambapo warembo kadhaa walimvaa jukwaani na kumng’ang’ania, huku wakionekana kuzungumza maneno ya kumshawishi kimahaba, lakini mkali huyo wa kibao cha Baadaye ‘aliwapotezea’.