Nay wa Mitego amesema baada ya kukamilisha ujenzi wa studio yake mpya iitwayo ‘Free Nation Production’ ameamua kumkabidhi producer wake Mr T Touch kama zawadi kutokana na kazi ambayo amekuwa akimfanyia katika muziki wake.
Akizungumza na Bongo5 jana, Nay amesema kuwa ameamua kufanya hivyo baada ya kuona kuwa muziki unazaolishwa na producer huyo unamwingizia pesa nyingi kuliko malipo anayompa.
“Wasanii tuna maproducer ,maproducer wetu tunajuaga kama wamekuwa hawaingizi kipato kikubwa sana tofauti na sisi wasanii,’ amesema Nay.
“Producer akikugongea ngoma moja ukimlipa laki tatu wewe unaweza ukaingiza zaidi hata ya milioni hamsini. Kwa producer aliyekufanyia hiyo ngoma inakuwa haimtoshi, for reel kabisa naongea kwa mara ya kwanza kwamba studio yangu imekamilika ambayo nampa zawadi producer wangu ambaye nilianza naye tangu… nasema nao mpaka leo hii ngoma yangu ya mwisho ya Mr Nay, zote hapa katikati amefanya yeye. Tumepata tuzo mara mbili, ni vitu ambavyo amefanya yeye, nimeingiza pesa nyingi lakini hela ambayo nilikuwa namlipa ni ileile laki mbili, laki tatu haimtoshi! Mimi nimeshaingiza zaidi ya milioni mia moja, mia mbili.”
“Kwahiyo nilichofanya nimekamilisha studio na nimemkabidhi kama zawadi yake. Studio inaitwa Free Nation Production. Mimi mwenyewe nitakuwa nafanyia kazi zaidi kwa sababu nahisi nitakuwa huru zaidi, japo kuwa sio lazima nifanyie hapo lakini hii ni kama zawadi kwa producer wangu, pia watu wengine wakihitaji kurekodi watarekodi.”
Bongo5