2:17 AM
Huu ndo muonekano wa ndani wa nyumba wa aliyekuwa manager wa msanii maarufu, Wema Sepetu aitwaye martin kadinda( picha chini), mwenyewe aniita manhattan ya Sinza.
Alipost hii picha juzi kwenye mtandao wa instagram baada ya kundi la watu kuibuka na kumtukana manager huyo kuwa hafai kuwa role model na maneno mengine machafu ambayo hayana maadili. Matusi hayo yalikuja baada ya manager huyo ku post picha yake huku akiwa ameacha kitovu chake nje.
Martin aliwajia juu watu hao na kuwaambia kuwa wengi wao wanaomponda mtandaoni hawana maisha wala elimu,hivyo wanachofanya ni kujifariji kama sio kujipooza machungu ya ugumu wa maisha kwa kumponda yeye (martin) ambaye anadai ana maisha mazuri kuliko hao wanaohangaika kumtukana mitandaoni wakati hata hawamjui.