Featured Posts

Wednesday, September 10, 2014

MAPYA YAIBUKA JOHARI NA RAY, SOMA ZAIDI HAPA

Na Rhoda Josiah
MKONGWE katika tasnia ya filamu Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’ ameonekana kuendelea kuteseka na penzi la mwigizaji Vincent Kigosi ‘Ray’ baada ya kunaswa akimzungumzia.
Mkongwe katika tasnia ya filamu Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’.
Tukio hilo lilijiri juzikati katika Viwanja vya Leaders Club kwenye uzinduzi wa filamu ya Mateso Yangu Ughaibuni ambapo Johari alikuwa amekaa na kruu yake (huku  wakigonga ulabu) ndipo mmoja kati wenzake hao, akagusia stori za Ray kisha Johari alicheka na kusema ipo siku Ray atarejea katika mikono yake.
Mkongwe katika tasnia ya filamu Bongo,Vincent Kigosi ‘Ray’.
“Ipo siku ambayo haijulikani tarehe wala mwaka Ray lazima atarudi katika mikono yangu kwani namfahamu sana Ray kuwa ni mtu wa kuruka lakini kwangu amefika,” alisikika Johari.

TUMEAMIA HUKU