Stori: Imelda Mtema
SIKU chache baada ya kufunga ndoa, mwigizaji Lucy Komba amempa sharti mumewe ambaye ni raia wa Dernmark, Janus Stanley Landrock kwamba hatozaa naye hadi atakapokamilisha suala la uraia wake.
SIKU chache baada ya kufunga ndoa, mwigizaji Lucy Komba amempa sharti mumewe ambaye ni raia wa Dernmark, Janus Stanley Landrock kwamba hatozaa naye hadi atakapokamilisha suala la uraia wake.
Akizungumza na paparazi wetu, Lucy alisema amemwambia mumewe akamilishe taratibu zote za nchini kwao ili yeye awe na uhalali wa kuishi nchini humo ndipo wazae watoto.
“Unajua napenda sana kuzaa hivi karibuni lakini itashindikana mpaka mume wangu atimize sharti la kupeleka vyeti vya ndoa na kuonyesha mimi ni mke wake halali nchini kwao na nitambulike kisheria,” alisema Lucy Komba.