Stori: Gladness Mallya
MWANAMUZIKI wa bendi ya Extra Bongo, Ramadhan Masanja ‘Banza stone’ amefunguka kwamba ndoa yake itafanyika kimyakimya na hakuna msanii atakayeshiriki.
MWANAMUZIKI wa bendi ya Extra Bongo, Ramadhan Masanja ‘Banza stone’ amefunguka kwamba ndoa yake itafanyika kimyakimya na hakuna msanii atakayeshiriki.
Akipiga stori na gazeti hili, Banza alisema ndoa yake haitakuwa na michango, kwani atamuita sheikh na watoto wa madrasa kwa ajili ya kupiga dufu, huku mama yake mzazi akiwa pembeni kama shahidi wakati atakapomuoa mchumba wake aitwaye Zubeda ambaye anaishi Tanga hivi sasa.
“Ndoa yangu haitakuwa na mbwembwe na itakuwa ya kikubwa zaidi, kwani hakuna msanii yeyote atakayeshiriki itakuwa ya kimyakimya tena asubuhi na mapema kwani sioni sababu ya kutangaza au kufanya sherehe kubwa,”alisema Banza.