Mwanamke mmoja ambaye alikuwa na ujauzito wa miezi mitatu nchini Pakistan amepigwa mawe hadi kufa nje ya jengo la mahakama kwa kosa la kuolewa na Mwanaume anayempenda badala ya mwanaume aliyechaguliwa na familia yake.
Kilichomkuta Farzana Parveen mwenye umri wa miaka 25 kinawakumba Wanawake wengi nchini Pakistan na katika nchi nyingine ambapo April 2014 Tume ya haki za binadamu nchini Pakistan ilisema Wanawake 869 nchini humo waliuwawa kwa namna hii nchini Pakistan.
Ferzana aliuwawa kwa madai ya kuiabisha familia yake ambapo mauaji hayo yamefanywa na cha kushangaza zaidi hata ndugu wa familia yake wameshiriki katika tendo hilo la kumuua.
Kikubwa kingine kilichohuzunisha ni kwamba Mwanamke huyu aliuwawa mbele ya Mahakama ambapo Baba mzazi wa Mwanamke huyu alijisalimisha Polisi baada ya kuhusika kwenye mauaji na kisha akasema hajutii kufanya hivyo kwa sababu ni aibu kubwa iliyoletwa kwenye familia na Marehemu.