Jaji wa Atlanta, Harold Murphy ametupilia mbali shitaka lililofunguliwa dhidi ya Nicki Minaj na aliyekuwa designer wake wa wig.
Katika shitaka hilo lilolofunguliwa February mwaka huu, Terrence Davidson alimtuhumu Onika Maraji (Nick Minaj) na mwenzake kwa kuvunja mkataba na ahadi ya kufanya majadiliano katika uzinduzi wa reality show aliyoianzisha kuhusu Wig na kutumia vibaya mitindo yake.
Mwanasheria wa Nicki Minaj aliiomba mahakama kutupilia mbali shitaka hilo kwa kuwa mlalamikaji alishindwa kutoa maelezo yenye mantiki.
Jaji Harold Murphy amekubali ombi la mwanasheria huyo na kueleza kuwa ni kweli malalamiko hayo yalikosa mashiko.