Featured Posts

Thursday, September 18, 2014

FIFA YATOA ORODHA YA UBORA KISOKA, TANZANIA YAZIDI KUDIDIMIA, WALES YAPAA

Timu ya taifa ya Wales, imeandika historia mpya baada shirikisho la soka duniani FIFA, kutoa orodha ya viwnago vya ubora wa soka vya mwezi huu kwa kuzingatia vigezo vya michezo ya kimataifa iliyochezwa siku za hivi karibuni.

Wales wameandiaha historia hiyo baada ya miaka 20 kupita ambapo wameonekana kukwea kwa nafasi 12 na kufanikiwa kuwakamata ndugu zao Sotland katika nafasi ya 29.
Mafanikio ya kupanda katika viwango hivyo vya ubora duniani yametokana na ushindi wa mabao 2-1 ulioshuhudia Wales wakiinyanyasa Andorra katika harakati za kuwania nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya barani Ulaya za mwaka 2016.
Kwa upande wa timu ya taifa ya Ireland ya Kaskazini imechupa kwa nafasi 24 na kukamata nafasi ya 71 ikiwa ni nafasi tisa nyuma ya Jamuhuri ya Ireland.
Timu ya taifa ya Uingereza imepanda kwa nafasi mbili ikitoka katika nafasi ya 20 hadi katika nafasi ya 18.
Jamuhuri ya Ireland imepanda katika viwango vya ubora kufuatia ushindi wao wa kwanza wa mabao 2-1 wakati wa kampeni za kusaka tiketi ya kucheza fainali za mataifa ya barani Ulaya dhidi Hungary, ili hali timu ya taifa ya Uingereza iliichabanga Uswiz mabao 2-0.
Mabingwa wa soka duniani timu ya taifa ya Ujerumani, imeendelea kusalia katika nafasi ya kwanza, kufuatia ushindi wa mabao mawili kwa moja walioupata dhidi ya Scotland walipoanza kampeni ya kuelekea nchini Ufaransa mwaka 2016.
Hata hivyo kabla ya mchezo huo, Ujerumani waliambulia kisago cha mabao manne kwa mawili mwanzoni mwa mwezi huu, kutoka kwa Argentina lakini haikuharibu mpango wa kuendelea kusalia kileleni mwa msimamo wa viwango vya ubora wa soka duniani.
Timu ya taifa ya Colombia nayo imepanda kwa nafasi tatu, ikiziacha timu za taifa za Uholanzi, Ubelgiji, Brazil, Uruguay, Hispania, Ufaransa pamoja na Uswiz zinazotengeneza orodha ya kumi bora.
Orodha kamili ya viwango vya ubora wa soka duniani ambavyo vimetolewa hii leo na shirikisho la soka duniani FIFA Bofya Hapa

TUMEAMIA HUKU