Featured Posts

Monday, August 25, 2014

Pellegrini asema ya moyoni kuhusu kurejea kwa Balotelli

Kurejea kwa mshambuliaji kutoka nchini Italia
Super Mario Barwuah Balotelli katika ligi ya nchini
Uingereza baada ya kusajiliwa na majogoo wa jiji
Liverpool, hakujamshtua meneja wa klabu bingwa
nchini humo Manuel Luis Pellegrini Ripamonti.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa
habari uliokuwa na mlengo wa mchezo wa hii leo,
Manuel Pallegrini amesema hatua ya kurejea kwa
mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24,
anaichukulia kama ilivyo usajili wa wachezaji
wengine waliojiunga na klabu zinazoshiriki ligi ya
nchini Uingereza.
Amesema hakuna asiyejua Balitelli alikuwepo Man
city na kisha alirejea nyumbani kwao Italia na
akajiunga na AC Milan na sasa amerejea tena
nchini Uingereza, hivyo kwa nini ichukuliwe kama
ni mshangao kwake? Alihoji mzee huyo kutoka
nchini Chile.
Pellegrini pia akaizungumzia tabia ya Mario
Balotelli kwa kuwaeleza waandishi wa habari
kwamba anamfahamu vyema na amekuwa na
wasifu wa kipekee hivyo haoni la ajabu zaidi.
Ikumbukwe kuwa hii leo ligi ya nchini Uingereza
itaendelea tena kwa mchezo mmoja ambapo Man
city watakuwa nyumbani Etihad Stadium wakicheza
dhidi ya majogoo wa jiji Liverpool waliomrejesha
Super Mario Barwuah Balotelli nchini Uingereza
kwa ada ya uhamisho wa paund million 16
akitokea AC Milan ya nchini Italia.

TUMEAMIA HUKU