Mbongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee’ au ‘Jide’ na Mtangazaji wa Radio Times FM, Gardner G Habash wakiwa katika picha ya pamoja.
Nyuma ya habari ya madai ya kuvunjika kwa ndoa ya Mbongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee’ au ‘Jide’ na Mtangazaji wa Radio Times FM, Gardner G Habash, kuna mambo mazito yameibuka, mara baada ya habari hiyo kuripotiwa na paparazi, Ijumaa ya wiki iliyopita.
Katika habari hiyo, ilielezwa kwamba mitandao mingi ya kijamii ndani na nje ya Bongo ilipambwa na sakata la mastaa hao kudaiwa kutengana huku Gardner akikanusha kwamba hakuna kitu kama hicho.
“Gardner atuambie ukweli maana hata huku nyumbani (Kimara-Temboni, Dar) tuna zaidi ya miezi miwili hatuwaoni,”
Ili kuthibitisha kilichosemwa, tulifika nyumbani kwa mastaa hao na kushuhudia geti na nyumba vikiwa na mavumbi ya kutotumika huku kukiwa hakuna hata alama za tairi za gari.Mapaparazi wetu walishinda eneo hilo bila wawili hao kurejea nyumbani ambapo kwa mujibu wa majirani, Gardner alionekana akiingia nyumbani hapo akiwa na gari aina ya Toyota Coaster la bendi yao ya Machozi na alipoondoka ndiyo ikawa kimoja.
“Ninyi angalieni mazingira. Ona maua na miti ilivyoweka vichaka na pori. Ni vigumu kuamini kama staa mkubwa kama Jide anaishi kwenye mazingira kama haya,” alisema mmoja wa majirani zao.
Tuliweka ‘patroo’ ya jirani huyo ambaye hadi tunakwenda mitamboni, wawili hao walikuwa hawaonekani nyumbani hapo.
Tuliweka ‘patroo’ ya jirani huyo ambaye hadi tunakwenda mitamboni, wawili hao walikuwa hawaonekani nyumbani hapo.
Pamoja na yote hayo na ishara mbaya zinazoonekana juu ya wawili hao ikidaiwa kila mmoja anaishi kivyake, bado Gardner amekuwa akisisitiza hakuna chochote kinachoendelea na kwamba hajui anayeeneza habari hizo ana lengo gani.
Kwa upande wake Jide, wikiendi iliyopita alitupia mtandaoni picha ya kidole chenye pete ya ndoa huku akiombwa chondechonde na mashabiki wake aendelee kutetea ndoa yake.