Featured Posts

Wednesday, August 20, 2014

MWANAMITINDO ALIYEPOTEA MAREKANI AKUTWA HOSPITALINI

Mwanamitindo raia wa Sudan aishie Marekani, Ataui Deng.
Mwanamitindo raia wa Sudan aishie Marekani, Ataui Deng aliyepotea kwa muda wa wiki mbili huku akitafutwa na polisi amekutwa akiwa hai katika hospitali moja New York.
Marafiki wa mwanamitindo huyo walitoa taarifa polisi na kuanzisha kampeni maalum ya kumtafuta baada ya kushindwa kumpata kwa kipindi kirefu, kampeni ambayo iliungwa mkono na watu maarufu akiwemo Rihanna.
Mpenzi wake, Grand Monohon alisema kuwa mara ya mwisho alimwambia kuwa anaaka kwenda mbali lakini aliacha simu na kila kitu chake nyumbani kwao.
Hakuna taarifa rasmi zilizotolewa  kuhusu hali ya Autui hadi sasa.
Kwa mujibu wa polisi, Ataui aliyeingia nchini Marekani kama mkimbizi akitokea kwao Sudan, alionekana kwa mara ya mwisho Agosti 6 majira ya saa tano usiku na kupatikana Agosti 18

TUMEAMIA HUKU