Mnanikosea! mwigizaji wa sinema za Kibongo, Mayasa Mrisho ‘Maya’ amefunguka kuwa watu wanaomsema kuwa amepotezwa kisanaa wanamkosea kwani anafanya sanaa kwa malengo.
“Sijapotezwa, kwenye sanaa kila mtu ana mipango yake, mimi sikurupuki, nafanya sanaa kwa malengo, hata sasa hivi nipo lokesheni Bagamoyo,” alisema Maya.