
Mtangazani Mahiri wa Redio 88.5 Clouds FM kupitia kipindi cha Jahazi, Ephrahim Kibonde akipingana na Askari wa Usalama barabarani wakati alipotakiwa kutii sheria bila shurti,mapema asubuhi hii jijini Dar es salaam.
Kibonde anadaiwa kusababisha ajali asubuhi hii eneo la Makumbusho, ikiwa gari aliyokuwa akiendesha kuigonga gari ya dereva mwingine kwa nyuma. Trafiki walifika eneo la tukio na kupima ajali, Kibonde alipoona hivyo akarudi nyuma na kuendesha gari lake kuondoka eneo la tukio bila kufuata taratibu za usalama barabarani.