Si kweli! Mtoto mzuri Bongo Movies, Jennifer Kyaka ‘Odama’ amekanusha vikali madai ya kutembea na pedeshee mmoja anayedaiwa kuwa ni mmiliki wa baa moja iliyopo maeneo ya River-Side, Ubungo jijini Dar.
Baada ya kusomewa madai hayo ambayo yamesambaa kwenye mitandao ya kijamii, Odama alikanusha vilivyo na kusema wanamsingizia tu.“Hee! Mbona huyo mtu wala simjui, ndiyo kwanza nazisikia hizo habari wakizikuza kwenye mitandao,” alisema Odama.
Kwenye madai hayo mtandaoni, Odama anadaiwa kuwa hajatulia na ndiyo sababu ya kutomwanika baba mtoto wake, jambo ambalo mwenyewe amesema si kweli bali ni utaratibu wa maisha yake aliojiwekea wa kutomuanika mzazi mwenzake.