Featured Posts

Monday, August 18, 2014

MUME WA MTU SUMU BINTI AMWAGIWA MARAGE YA MOTO KISA. MUME WA MTU

Mke
wa mtu, Mwajuma Prima amelazwa
Hospitali ya Mkoa wa Morogoro baada ya
kumwagiwa mwilini sufuria la maharage
yalitokuwa yakichemka jikoni, kisa
kupeleka maneno ya umbeya kwa mume
wa mtu.
Tukio hilo la kusikitisha lilijiri juzikati
majira ya saa 12:00 jioni ambapo
mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la
Fatuma ndiye anayehusishwa na msala
huo uliotokea nyumbani kwake maeneo
ya Mtaa wa Ndege, Msamvu mjini
Morogoro.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo
walidai kwamba, siku ya tukio, Fatuma
alimshutumu Mwajuma kuwa amekuwa
akimwambia mumewe maneno ya
umbeya ili kuwatenganisha.
“Huyu Mwajuma anaishi Kihonda, kila
baada ya siku tatu anakuja kwenye
nyumba hii kumsalimia mama yake
mdogo.
“Juzi Fatuma aligombana sana na mumewe
na chanzo cha ugomvi huo ilidaiwa kuna
mambo mwanaume huyo aliambiwa na
Mwajuma.
“Mwajuma alipofika kwa mama yake
mdogo ndipo Fatuma akamkwida na
kumuuliza kwa nini alimwambia mumewe
mambo ya umbeya?
“Mabishano yalishika kasi na mwishowe
walipigana. Fatuma alipoona amezidiwa,
akaingia jikoni na kuipua sufuria la
maharage yaliyokuwa yakichemka na
kumwagia Mwajuma mwilini,” alisema
mmoja wa majirani aliyeomba hifadhi ya
jina lake. Akizungumza na mwandishi, mama
mdogo wa Mwajuma alisema:
“Fatuma ni ndugu yetu, tunatoka naye
kijiji kimoja Turiani. Ni kweli alimmwagia
Mwajuma maharage ya moto mwilini.
“Fatuma alikuwa anamshutumu
mwanangu kumchonganisha na mumewe
ndipo walipoanza kupigana.
“Fatuma alipoona kazidiwa aliingia jikoni
akaipua sufuria la maharage yaliyokuwa
yakichemka wna kummwagia mwanangu
mwilini na kumsababishia majeraha
makubwa.”
Mume wa Mwajuma, Peter Muhanda
alikiri mkewe kupatwa na masaibu hayo
na kwamba alitoa taarifa polisi ambapo
mtuhumiwa alikamatwa.

TUMEAMIA HUKU