Video model Agnes Masogange mwaka jana alitawala vyombo vya habari baada ya kukamatwa na polisi huko South Africa akiwa na mwenzake Melisa Edward wakiwa na mzigo wa Crystal Methamphetamine wenye thamani ya Tsh bilioni 6.8.
Taarifa mpya kutoka kwa kamanda wa polisi kitengo cha kuzuia na kupambana na dawa za kulevya Gedfrey Nzowa inasema kikosi hicho kilimshikilia Masogange usiku wa juzi baada ya kurejea akitokea South Africa. Taarifa inasema kwamba Masogange alihojiwa kwa zaidi ya masaa 10 na kupekuliwa na baadae kuachiwa hutu bila masharti.
Masogange alivyotafutwa kwenye simu alijibu kwa kifupi na kusema,”Hilo unalosema siyo kweli na sipo tayari kuzungumzia. Siwezi kuzungumza na chombo cha habari kwa sasa, shida yako nini”.
Source : Mwananchi
Milioni 392 Zajenga Barabara HEWA Dar es Salaam
-
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob amebaini matumizi ya Sh392
milioni zilizoandikwa kwenye taarifa ya manispaa hiyo kuwa zimetumika kwa
ajili y...





