This is default featured slide 1 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
This is default featured slide 2 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
This is default featured slide 3 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
This is default featured slide 4 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
This is default featured slide 5 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
Sunday, August 31, 2014
HATIMAYE UPEPO UMEGEUKA KAJALA SASA ANA PESA CHAFU, KUMUAJIRI WEMA,
Habari za ‘ufukunyuku’ zinadai kwamba, kwa utajiri alionao kwa sasa, Kajala anaweza kudiriki kumwajiri Wema kama kisemavyo chanzo.
Kwa mujibu wa chanzo makini kilicho karibu na wote kwa maana ya kutafuna pande zote, mwigizaji huyo ambaye enzi za ushosti wake na Wema alikuwa akionekana kama kijakazi, sasa fedha imemtembelea kiasi cha kutosha wakati mwenzake kwa bahati mbaya eti ‘anatembelea ringi’.
Chanzo kilisema kwamba Kajala kwa sasa ana maisha ya ‘kitonga’, amepanga kwenye nyumba nzuri ya ghorofa, ana kampuni yake ya filamu (KAY Entertainment), magari manne, anatembea na wapambe (walinzi) huku akaunti yake benki ikiwa imetuna.
“Yupo vizuri, anamiliki ofisi kubwa ya kuzalisha sinema, magari mawili ya ofisi pamoja na magari mawili ya kutembelea (Brevis na Harrier) na anaishi katika nyumba anayolipa kodi kwa mwezi dola 2,000 (zaidi ya Sh. milioni 3.2),” kilidai chanzo hicho na kudai kwamba si mbaya Kajala akamkumbuka mwenzake hata kwa kumwajiri kwenye kampuni yake.
Akizungumza na waandishi wetu, Kajala alisema anamshukuru Mungu kwani fedha hizo amezizalisha kupitia kazi zake pamoja na biashara mbalimbali alizokuwa akizifanya, hajahongwa na mtu yeyote.
“Sijahongwa na mtu yeyote, kila mtu ana akili zake katika kutafuta fedha, nafanya biashara huku nikiigiza sinema zangu na Mungu amenijalia mambo yanakwenda vizuri,” alisema Kajala.
Kuhusu kumwajiri staa mwezake huyo, Kajala hakutaka kulizungumzia hilo.
Utafiti uliofanywa na Ijumaa Wikienda umebaini kwamba Wema aliyemlipia Kajala Sh. milioni 13 asiende jela mwaka jana, ambaye kipindi kifupi kilichopita alikuwa na kampuni ya kuzalisha sinema, wapambe, akaunti iliyonona benki, magari ya kifahari ya kutembelea na samani nyingine, nyingi zimepotea kama si kuyeyuka kabisa.
Kama hiyo haitoshi, ilidaiwa kuwa hata akaunti benki haijanona na hata wapambe wa kutembea naye wameyeyuka.
Ili kutaka kujua anazungumziaje ‘challenge’ hiyo ya kudaiwa kuporomoka kiuchumi, wanahabari wetu walimtafuta Wema kwa siku tatu mfululizo lakini hakupatikana huku simu yake ikiita muda mrefu bila kupokelewa.
Akizungumza na waandishi wetu kwa sharti la kutoanika jina gazetini, rafiki wa karibu wa Wema alikiri kuwa staa huyo mwenye nyota isiyochuja, ameshuka kiuchumi tofauti na enzi zile ambazo walikuwa wakitanua katika viunga mbalimbali na msururu wa watu huku Madam akisimamia shoo nzima ya malipo.
Hivi karibuni, baadhi ya mashabiki wa Wema ambao wanajiita Team Wema, walimuonya staa wao huyo wakidai ananyonywa na mpenzi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambaye pia amekuwa akimdhalilisha katika majukwaa pindi anapofanya shoo zake.
Walimtaka abadilike kwani yeye ndiye mwenye nyota ya kung’aa lakini Diamond ananufaika yeye peke yake na muziki wake.
Baada ya Diamond kushambuliwa na Team Wema, naye alitoa majibu ambayo yalionesha dhahiri kwamba ndiyo sababu inayomfanya Wema ashuke kisanaa na kiuchumi.
NOMA GARI LA MSANII DUDE LAIBUA MAZITO MAPYA KABISAA
Akizungumza na mwanahabari wetu kwa njia ya simu kutoka Meatu mkoani Simiyu, Samson ambaye ni mume wa Lily alisema alistaajabu aliposikia Dude akisema gari ni lake wakati ni la mkewe aliyefunga naye ndoa mwaka 2011 na yeye alishiriki kulinunua.
“Isitoshe katika vijana waliokamatwa na gari hilo, mmoja ni mdogo wa mke wangu na siri zote za yeye kutoka na Lily huwa ndugu zake wananisimulia.
Baada ya madai hayo kuwa ‘hoti’, Ijumaa Wikienda lilimsaka Lily ambaye hakuwa tayari kuzungumza kama gari hilo ni lake au la Dude na kusisitiza aulizwe Dude ambaye alikiri kufahamiana naye huku akikubali kumfahamu Samson pia.
“Nimejaribu kumsaidia kisanii, sitaki kuchafuka, Lily ni mwanangu nimemlea,” alisema Dude
WAREMBO KAMA NANE HIVI WACHEZEA KICHAPO KIKALI USIKU WA MANANE
INAUMA SANA! MFANYABIASHARA AMCHARANGA MAPANGA ALBINO
“Nilikuwa nimelala, ghafla nikasikia mtu akiingia akiwa ameshika panga na kuanza kunikatakata huku akitaka kuninyofoa masikio yangu. Nilimtambua kuwa ni Lyimo ambaye ni jirani yetu.”
Alisema kuwa kutokana na woga alioupata, aliogopa kulala hivyo alikimbilia kwa mjumbe wa mtaa wao, Filemon Gyuna ambako alipatiwa huduma ya kwanza.
Kwa upande wake, mwenyekiti wa Chama cha Maalbino Mkoa wa Morogoro, David Mganga alisema: “Natoa wito kwa jamii ielewe kuwa kiungo cha albino hakiwezi kumpa mtu utajiri au mafanikio, waache kututesa sisi maalbino.”
MWIMBAJI WA TAARABU WA BONGO ANUSURIKA KUUAWA NA AL SHABAAB HUKO MOMBASA
Oooh nooo ! Mwimbaji na Kiongozi wa Kundi la
Mashauzi Classic , Aisha Ramadhani ‘ Isha
Mashauzi’ , amejikuta kwenye wakati mgumu
baada ya kuvamiwa na kundi linalojiita Al -
Shaabab ( siyo wale orijino wanaosifika kwa
ugaidi ).
Mwimbaji na Kiongozi wa Kundi la Mashauzi
Classic , Aisha Ramadhani ‘ Isha Mashauzi ’ .
Tukio hilo ambalo liliibua sintofahamu kwa
wananchi , lilitokea juzikati katika hoteli
inayojulikana kwa jina la Grassovila iliyopo
Mombasa nchini Kenya ambapo walimuibia
msanii huyo kila kitu alichokuwa nacho .
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Isha
alisema kuwa alikwenda Mombasa kwa ajili ya
mwaliko wa mashabiki wa Timu ya Arsenal ya
England waishio Mombasa na alipokuwa
akijiandaa hotelini, ghafla alishtukia watu
waliojificha nyuso wakiingia katika chumba
alichokuwepo kisha kumuamuru atoe kila kitu.
“ Nilishtuka sana kuona kundi la watu likivamia
chumbani kwangu , nasikia walianzia katika
vyumba vingine , jamaa walinichukulia kila kitu
nilichokuwa nacho hadi hati ya kusafiria lakini
namshukuru Mungu Watanzania wenzangu
walinisaidia na kuweza kurejea Bongo,”
alisema Isha .
Alisema polisi nchini humo wanaendelea
kufanya uchunguzi kwa ajili ya kuwatia hatiani
‘ wahuni’ hao.
Hadi Isha anafanikiwa kurudi Bongo, hakuna
mtu yeyote ambaye alikamatwa kuhusiana na
tukio hilo.
KUHUSU TUUMA ZA KUMRISHA DIAMOND VIPORO KILA SIKU.. WEMA AFUNGUKA .. SOMA HAPA ALICHOJIBU
MAHABATi ! Beautiful Onyinye wa Bongo,
Wema Sepetu ‘ Madam’ amedhihirisha kuwa
yeye ni mwanamke tayari wa kuwekwa ndani
baada ya kusema anajitahidi kila siku katika
suala la mapishi ili asimlishe viporo mwandani
wake, Nasibu Abdul , ‘ Diamond’ . Akipiga domo na paparazi wetu , Wema
alisema kama mwanamke anajua thamani ya
mwanaume siku zote hata kama ‘ baby ’ wake
atarudi usiku , lazima aingie jikoni kupika na
haweki chakula kwenye ‘ hot pot ’ .
“ Siku zote si kwamba najisifia ila kwa jikoni
ndiyo mwenyewe sasa kwa nini nipike chakula
halafu niweke kwenye hot pot ? Kwangu
siruhusu kabisa itokee , ” alisema Wema .
HII KALI. WAZIRI MKUU PINDA AWAKIMBIA WAANDISHI WA HS
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda jana
alilazimika kutumia mlango wa uani
kuondokea badala ya ule mkuu kwa kile
kinachohisiwa kuwakwepa waandishi wa
habari waliokuwa wakifuatilia ufunguzi
wa mkutano wa mawaziri wa mambo ya
nje na mazingira kutoka nchi za Afrika.
Pinda ambaye alikuwa akifungua
mkutano huo, aliondoka mara tu baada ya
kumaliza shughuli iliyompeleka huku
akiacha kushiriki tukio la kupiga picha
lililoandaliwa kwa ajili yake upande wa
lango kuu wa ukumbi huo ambako
waandishi walikuwa wakimsubiri kwa
ajili ya kufanya naye mahojiano.
Awali wakati Pinda akihutubia mkutano
huo uliokuwa ukifanyika katika Ukumbi
wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam,
baadhi ya maofisa wa itifaki walionekana
wakisimamia zoezi la kupanga viti kwa
ajili ya tukio la picha ya pamoja ambalo
Waziri Mkuu huyo kama mgeni rasmi
ilitakiwa ashiriki.
Ni maofisa hao pamoja na baadhi ya
watumishi wa idara zinazohusika na
mkutano huo, ndio waliowaelekeza
baadhi ya waandishi wa habari ambao
hawakubahatika kuingia ndani kusubiri
katika eneo hilo la lango kuu ili waweze
kufanya mahojiano na Pinda hata hivyo
ahadi hiyo haikutimia.
Hatua hiyo ndiyo iliyoibua hisia kwamba
huenda, Pinda alifanya hivyo kukwepa
maswali ya waandishi wa habari hasa
kutokana na kuwepo kwa taarifa
zinazodai kuwa ametangaza dhamira yake
ya kuwania ukuu wa dola mwaka 2015.
Tangu taarifa hizo ziripotiwe kwa mara ya
kwanza na vyombo vya habari Jumapili
iliyopita, si Pinda wala wasaidizi wake wa
karibu ambao walijitokeza kuthibitisha
juu ya taarifa hizo.
Kutokana na hilo vyombo vya habari
nchini vimekuwa vikimtafuta Pinda ili
aweze kuzungumzia habari hizo, ambazo
anadaiwa kuzitoa mbele ya wajumbe wa
Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM) Taifa kutoka mikoa ya Kanda ya
Ziwa aliokutana nao Ikulu ndogo ya jijini
Mwanza, Jumamosi iliyopita.
Katika tukio la jana wakati waandishi
wakimsubiri nje ya lango kuu, Pinda
alionekana akishuka chini na kuingia
katika eneo la pembeni ya ukumbi,
ambako inasemekana eneo hilo lina
mlango wa nyuma wa kutokea nje ya
ukumbi.
Waandishi hao, kwa matumaini
waliendelea kumsubiri Pinda kwa zaidi
ya dakika kumi bila mafanikio, huku viti
vilivyoandaliwa kwa ajili ya picha ya
pamoja vikiwa vimetelekezwa na
mkutano ukiendelea kama kawaida ndani
ya ukumbi huo.
Baada ya muda alijitokeza kijana ambaye
inasemekana ni mmoja wa wafanyakazi
kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais
Mazingira akisema kuwa; “Jamani
tuliwaalika watu wachache Waziri Mkuu
ameshamaliza na ameondoka, kama kuna
mtu hajamsikiliza Press release (taarifa ya
vyombo vya habari) ya Waziri Mkuu ipo
akatoe ‘photocopy’ karatasi ipo kwa yule
dada, (huku akionyesha mmoja kati ya
waandishi waliokuwa ndani ya ukumbi na
kwa wale wa Tv naomba mchukue kwa
kaka pale wa Tumaini.”
Akiwa mkoani Mwanza wiki iliyopita,
Pinda anadaiwa kuwaeleza wajumbe hao
wa CCM kuwa ameamua kuwania nafasi
ya Urais baada ya kushawishiwa na
viongozi wakuu wastaafu na viongozi wa
dini.
HATARI SANA: WASANII WAANDAMANA NUSU UCHI NCHINI KENYA..JIONEE MWENYEWE HAPA!
Nchi jirani ya Kenya matukio kama haya yamekua mengi pia lakini hawa ndio wamechukua headlines kwa kuwa Wanamuziki wa kwanza kuandamana kwa aina hii.
Ripota wa TZA Kenya Julius Kepkoich amesema Wasanii hawa waliandamana nje ya ofisi za Nation Media Nairobi wakiwa nusu uchi kulalamikia nyimbo zao kutochezwa na vyombo vya habari.
Wakiwa na mabango yao Wasanii hawa kutoka maeneo ya Vitongojini walisema wanaumizwa na kitendo cha nyimbo zao kutochezwa, wamekua wakitoa nyimbo mpya kila wakati lakini hazichezwi kwenye Radio wala TV badala yake zinazochezwa ni za wasanii walewale kila siku.
HABARI KAMILI: WATU KUMI WAMEFARIKI DUNIA NA MAJERUHI SABA KATIKA AJALI MBAYA ILIYOTOKEA MBALIZI
PENZI LA MAINDA LAGOMBEWA NA WANAUME KIBAO SOMA ZAIDI HAPA
Staa wa Filamu za Kibongo aliyeamua kumpokea Yesu, Ruth Suka 'Mainda' amesema amekuwa akipata wakati mgumu kumjua mwanaume wa kweli ni yupi ambaye anaweza kumuoa na ndoa yake ikawa na raha badala ya majuto kama ilivyo kwa baadhi ya wasanii wenzake....
TUMEAMIA HUKU
-
Milioni 392 Zajenga Barabara HEWA Dar es Salaam - Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob amebaini matumizi ya Sh392 milioni zilizoandikwa kwenye taarifa ya manispaa hiyo kuwa zimetumika kwa ajili y...