Na Shakoor Jongo
STAA katika tasnia ya filamu Bongo Wema Issac Sepetu leo atatinga Uwanja wa Taifa kushuhudia mechi ya mwisho ya Simba na Yanga baada ya hapo atachukuwa nafasi hiyo kwenda kumdai Mrisho Ngasa mpira wake.
Akizungumza na Championi Jumamosi katika ofisi za gazeti hili zilizopo Bamaga jijini Dar, Wema alisema hajawahi kwenda uwanja wa taifa kuangalia mechi ya aina yoyote ile zaidi ya mabonanza yanayohusisha timu za Bongo Muvi lakini Jumamosi hii atafanya hivyo nia na madhumuni kwenda kumdai Mrisho Ngasa mpira wake aliyedai atampa zawadi baada ya kupiga ‘hat trick’.
“Kiukweli sina mazoea kivile na Ngasa lakini watoto wa ndugu zangu huwa wananisumbua wakitaka mpira ambao wanadai walisoma katika gazeti kuwa Ngasa amenipa zawadi ya mpira sasa nimeamua nihudhulie mechi hiyo baada ya mtanange kuisha namfuata akanipe mpira wangu kwani nimesikia Jumamosi ndio mwisho wa ligi naamini sitakuja kumuona tena,” alisema Wema.
Gazeti ndugu na hili Championi Jumatano liliwahi kuripoti habari kuwa zwadi ya mpira aliopata Ngasa atampa Wema.