Afrika Kusini ni nchi yenye uchumi mkubwa Afrika
ambao umevutia Waafrika wengi kukimbilia huko
kwa ajili ya kufanya kazi kama za Udereva, uuzaji
mafuta kwenye vituo vya mafuta pamoja na kazi
nyingine mbalimbali.
Taarifa kutoka kwenye mji wa Pretoria ni kwamba
Watanzania ambao wanamiliki na kufanya biashara
mbalimbali zikiwemo za Maduka na wale
wanaomiliki hoteli, wamevamiwa wakiwa kwenye
mali zao na kufanyiwa uharibifu na nyingine
kuchomwa moto.
Ni kundi la watu ambalo linaendeleza uvamizi huu
ambapo linawashutumu Watanzania hawa
kuhusika na biashara ya dawa za kulevya, yani
kwa ufupi Watanzania wanasema hata kama kweli
wangekua wanafanya hii biashara, walio na
mamlaka ya kuwavamia ni Polisi na sio hao raia.
Inaaminika kundi hili lina sehemu kubwa ya
madereva Taxi wazawa wa nchi hiyo ambao
wamekua wakiumizwa na jitihada za raia wa
kigeni wa Nigeria na Watanzania ambao
wamejazana kwenye mtaa wao wakimiliki maduka
mbalimbali yakiwemo ya nguo pamoja na hoteli.
Tayari balozi wa Tanzania amekutana na
Watanzania hao na kuahidi kulifatilia ambapo ni
Watanzania watano wamejeruhiwa wakiwemo
watatu ambao bado wako hospitali na mmoja wao
kavunjika mkono, mmoja kapigwa kichwani.
Kabla ya Watanzania wengine kuwahi kufunga
maduka yao, maduka matatu ya Watanzania
pamoja na hoteli mbili zinazomilikiwa na
Watanzania zilivamiwa na wakachuchukuliwa simu
na watu kupigwa ambapo polisi walipokuja
hakuna chochote kilichofanyika zaidi ya maelezo.
Picha hizi zote zilipigwa na Mtanzania akiwa
anakimbia baada ya kufanikiwa kufunga duka lake