Featured Posts

Monday, June 9, 2014

TAZAMA PICHA MAMIA WAMIMINIKA KUMZIKA MZEE SMALL MAKABURI YA SEGEREA

Mwili wa Marehemu Mzee Small ukihifadhiwa kwenye nyumba yake ya milele jioni ya leo katika makaburi ya Tabata Segerea jijini Dar.
Ustadhi akimuombea marehemu dua ya mwisho baada ya kuuhifadhi mwili wake kaburini.
Msanii wa kundi la Vichekesho Orijino Komedi, Emmanuel Mgaya 'Masanja Mkandamizaji',akiweke udongo kwenye kaburi la mzee Small.
Mdogo wa marehemu mzee Small akiwa chini baada ya kuzidiwa na kuishiwa nguvu muda mfupi baada ya shughuli za kuhifadhi mwili wa kaka yake kumalizika.
Jeneza la Mzee Small likiombewa.
  Jeneza likipelekwa kwenye gari.
...Llikiwekwa ndani ya gari.
Jeneza likishushwa makaburini.
   Safari ya kuelekea makaburini.
Meneja wa Global Publishers, Abdallah Mrisho (mwenye tai na miwani katikati) akiwa na baadhi ya wasanii waliofika kwenye maombolezo.
Mahmoud Said Ngamba akisoma wasifu wa baba yake.
   Waombolezaji waliojitokeza msibani.
   Rais Kikwete alipowasili msibani.
Rais Jakaya Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo pembeni (kulia) ni Mahmoud, mtoto wa marehemu.
  Rais wa Shirikisho la Filamu nchini (Taff), Simon Mwakifwamba akisalimiana na Rais Kikwete.
Mzee Chillo akiteta jambo na Rais Kikwete.
  Rais Jakaya Kikwete akiteta jambo na Mwenyekiti wa Bongo Muvi, Steve Nyerere, na mtoto wa marehemu Mahmoud (aliyevaa kibaraghashia).
Wananchi wakisalimiana na Rais Kikwete.
UMATI wa watu umejitokeza katika kumuaga marehemu Said Ngamba 'Mzee Small' nyumbani kwake Tabata-Kimanga na mazishi kufanyika katika makaburi ya Segerea, jijini Dar es Salaam.

TUMEAMIA HUKU