Featured Posts

Monday, June 9, 2014

MKE WA CHARLZ BABA AMDUNDA MKE MWENZA MAKOFI CHOONI, SOMA ZAIDI HAPA

Mke  halali  wa Rais  wa  bendi  ya  mashujaa  musica  Charles  Gabriel  Cyprian  ‘Chaz Baba’, Rehema  Sospeter  Marwa  mwishoni  mwa  wiki  jana  alizua  timbwili  la  mwaka  baada  ya  kumchapa makofi  msichana  mmoja  ajulikanaye  kwa  jina  la  Husna….

Tukio  hilo  lililoshuhudiwa  na  mwandishi  wetu  lilitokea  majira  ya  saa  nane  za  usiku  katika  ukumbi  wa  Letas ( zamani Busness Park)  uliopo  Makumbusho  wakati  bendi  ya  Mashujaa  ilipokuwa  inatoa  burudani.
Sakata  zima  lilikuwa  hivi;Husna  alikuwa  anakunywa  kwenye  Pub  hiyo , mara  akatokea  mke  wa  Chaz Baba  na  kumfuata kaunta  Husna  na  kumwambia  amependeza  sana  kwa  pamba  alizotupia  kisha  akamuomba  amsindikize  chooni.
CHAZ BABA
Wakati  wanaongea, mwandishi  wetu  aliwasikiliza  na  kuanza  kuwafuatilia  hadi  chooni. Walipofika  chooni  Rehema  alimkunja  Husna  na  kumwambia  kuwa  yeye  ni  mke  halali  wa  Chaz  Baba  hivyo  anamuomba  aachane  na  mume  wake  lasivyo  atamng’oa  meno….
“Sikia  nikwambie  wewe  binti, mimi  ndo  mke  halali  wa  Chaz  Baba, hivyo  nakuomba  kiustaarabu  uachane  na  mume  wangu  lasivyo  utahama  mjini  bila  kupenda, “ alisikikia  akisema  Rehema  huku  akiwa  amemkwida  Husna.
Hata  hivyo  Husna  alijitetea  kwamba  hana  mahusiano  na  Chaz Baba  kwani  walishaachana  muda  mrefu  na  kumtaka  Rehema  asikurupuke….
“Nisikilize  wewe  mwanamke, siku  nyingine  usiwe  unakurupuka  kama  kichaa, kuolewa  unajiona  umefika  ee!!  Sasa  kwa  taarifa  yako  huyo  Chaz  baba  nilishamtema  kitambo  tu, achana  na  mimi, hangaika  na  wengine…..Kwanza  jichunge  wewe  mwanamke,”  alisikika  akisema  Husna.

Kauli  hiyo  ilimkera  Rehema  na  kumtia  Nakozi  mbili  za  moto ( makofi  mawili adimu)  Husna  aliyekuwa  amevalia  kigauni  cha  rangi  nyekundu  kisha  akaondoka  na  kurudi  kupata  kilaji  ndani  ya  Pub  hiyo  wakati  mumewe  akiendelea  kutumbuiza….
Baada  ya  tukio  hilo, mwandishi  wetu  alimfuata  Rehema  ambaye  alikuwa  na  wapambe  wa  kutosha  na  kumuhoji  kulikoni  kupigana  chooni..!!!!??
“Ndo  ivo, nshamtandika  vibao, nilikuwa  nampa  onyo  aachane  na  mume  wangu, ni  hilo  tu,”  alijibu  Rehema.
Husna  aliporudi  ukumbini  alianza  kuelezea  tukio  zima  lilivyokuwa  hadi  kuchapwa  makofi, “Mimi  namshangaa  sana  yule  mwanamke, yaani  kiukweli  Chaz  Baba  nshafanya  naye  mapenzi  siku  nyingi  na  nimeshaachana  naye. Sasa  namshangaa  anakuja  kuniuliza  leo  na  kunipiga  chooni, ila  we  acha  tuu, kuna  kitu  ntamfanyia, asidhani  namwogopa,” alisema  Husna.

TUMEAMIA HUKU